KUHAKIKISHA NYUMBA ZA SHIRIKA ZINAKUWA SALAMA NA ZINALIPIWA KODI

 

Mkuu wa wilaya mjini ndugu marina joes thomas amewataka masheha kulisaidia shirika la nyumba zanzibar kuhakikisha  nyumba za  shirika hilo zinakuwa salama na zinalipiwa kodi.

Akifunguwa semina ya siku moja kwa masheha wa mkoa mjini  magharibi katika kituo cha elimu mbadala rahaleo mjini zanzibar juu ya uhumimu wa kutunza nyumba za maendeleo za serikali ndugu mrina amesema masheha wanapaswa kuhakikisha  nyumba hizo haziishi watu ambao hawakupagishwa na serikali.

Mkuu huyo wa wilaya amesema serikali imejenga nyumba hizo ili kuona wananchi wake wanaishi katika mazingira bora ili wafaidike na matunda ya kuwepo serikali yao hivyo kuzitunza liwe ni jambo la lazima.

Mkurugenzi  kuu wa shirika la nyumba zanzibar ndugu riziki jecha salum  amesema nyumba za shirika lake zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya wapagaji kuzitumia vibaya  na kukwepa kulipa kodi.

Mwanasheria wa shirika hilo ndugu majda makame othman amewataka masheha kufuatilia matumizi mazuri ya nyumba hizo kwani nyengine zinatumika vibaya kwa kudfanyiwa uchafu,kuvunjwa na kufanywa madanguro.

Kwa upade wao masheha hao waeliomba shirikala nyumba kubadilisha sheria zake za ukodishaji wa nyumba zake zilioko katika maeneo mbali mbali ya unguja na pemba