KUHAKIKISHA SHERIA ZINAZOREKEBISHWA ZINAWEZA KUTEKELEZEKA.

 

Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria jaji mshibe ali bakar  amewataka wananchi kuendelea kuishauri tume yake ili kuhakikisha  sheria zinazorekebishwa  zinaweza kutekelezeka.

Jaji mshibe amesema sheria ya mufti inafanyiwa marekebisho kwa lengo la kumpa nguvu katika kutekeleza majukumu ya ofisi hiyo ambayo awali yamekosekana.

Amesema hayo huko tunguu katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa kusini unguja wakati tume ya kurekebisha sheria ilipokuwa ikikusanya maoni kuhusu marekebisho ya sheria ya ofisi ya mufti na sheria ya umiliki wa ardhi.

Wakitoa maoni yao wananchi wa mkoa wa kusini unguja wamesema   kunakosekana kwa elimu ya kutosha kwa jamii jambo ambalo ni kikwazo katika utekelezaji wa sheria.