KUHAKIKISHA WATOTO NJITI WANAPATIWA HUDUMA MUHIMU.

 

 

 

Waziri mwa kazi uwezeshaji wazee ,vijana wanawake na watoto mhe, modline castico amewataka wazazi  wenye watoto waliozaliwa chini ya miezi saba wametakiwa kushirikiana  kuhakikisha  watoto wao wanapatiwa huduma  muhimu.

Akizungumza  katika maadhimisho ya siku ya mtoto njiti  duniani  castico amesema  watoto wanaozaliwa katika hali hiyo wanahitaji matunzo ya kutosha na kwamba baba na mama lazima washirikiane ili kuona watoto hao wanahudumiwa vyema.

Amesema  kuna ongezeko kubwa la watoto wanaozaliwa na tatizo hilo na kuserikali kwa kufahamu hilo  imejipanga kuwapatia huduma za afya zinazostahili kwa watoto hao.

Naye  mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto duniani  unicef dokta  oluwatosin kuti  amesema   jamii inapaswa kufanya kazi kwa pamoja  kuondoa   matatizo mbali mbali  kwa mtoto njiti ili kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Dokta   maulid abdala wa hospitali ya mnazi mmoja  amesema  kuwa zipo  sababu nyingi zinazochangia  kuongezeka kwa kuzaliwa watoto njiti ikiwemo   upungufu wa damu mwilini , uzazi katika  umri mkubwa.

Kwa upande wa mama mtoto njiti ameelezea  changamoto mbali mbali zilizomkuta wakati akimlea mtoto huyo .

muhudumu wa kitengo ya maradhi hayo kutoka hospitali ya mnazimoja  anaelezea  matatizo amesema mtoto njiti anapozaliwa hahitajiki kuchuliwa na  mtu  zaid ya mama.