KUHAMASISHA UMUHIMU WA AFYA YA UZAZI NA MALEZI BORA KWA WAZAZI NA JAMII

Mkurugenzi idara ya maendeleo ya wanawake na watoto zanzibar nasima hajichumu amesema miongoni mwa mikakati ya kudhibiti kuongezeka kwa matukio ya udhalilishaji kwa watoto ni kuhamasisha umuhimu wa afya ya uzazi na malezi bora kwa wazazi na jamii
akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kitaifa ya mtoto wa kike duniani zilizofanyika huko mazizini ikiwa lengo ni kuweka usawa na kuondosha ubaguzi dhidi ya watoto na kuweka usawa wa kijinsia na kuona wanapata haki sawa na elimu bora itayowawezesha kujitambua
amesea kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji na mimba za umri mdogo ni miongoni mwa sababu zinazochangia vifo wakati wa kujifungua ,kusababisha matatizo ya kiafya kwa watoto ambao watabeba ujauzito mapema
amefahamisha kuwa katika kupambana na vitendo hiyo serikali iimezindua mpango maalum wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watito ili kuona jamii inahamasika juu ya umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi pamoja na kujiwekea mikakati ya k udhibiti kuongezeka kwa matukio ya udhalilishaji
Akisoma risala ya maadhimisho ya siku hiyo mwenyekiti wa bodi ya washauri ya watoto zanzibar jafar ahmada bakari amesema uwepo wa sikuku hiyo kwao ni kuona vipi serikali na taasisi mbali mbali zinavyothamini na kuguswa na matukio mabaya yanayowakuta watoto katika maeneo yao
akitoa nasaha kwa watot hao bibi molin nenson kutoka save the child ren amesema takwimu zinanaonesha kuwa watoto zaidi ya asilimia hamini duniani hufanyiwa vitendo vywa udhalilishaji hiyo kuna kila sababu ya kuchukuwa tahadhari na kupiga vita vitendo hivyo
maadhimisho hayo yalipambwa na mchezo maalum wa mtoto wa kike kongamano la wanafunzi la udhalilishaji pamoja na washiriki kuguswa na historia zililizotolewa na na mtoto awena hassan seif ambae ni mlemavu wa macho pamoja na suhayla msham abae kwa sasa anaishi na maabukizi ya virusi vya ukimwi na kutoa wito kwa jamii https://youtu.be/WXrSlO_qfLAambapo ujumbe wa mwaka huu ni elimu ni mafanikio kwa mtoto wa kike