KUHARIBU MINDOMBINU YA VISIMA VYA KUSMBAZIA MAJI

 

Mamlaka ya maji zawa imesikitishwa na vitendo vilivyofanya na watu wasiojulika kwa  kuharibu mindombinu ya visima vya kusmbazia maji katika eneo la kiashange mkoa wa kaskazini a unguja.

afisa uhusiano wa mamlaka ya maji zawa zahoro sulemain alifika katika tukio hilo     ambapo  alisema kitendo cha kukata waya za arthingi katika visima vya kusambazia maji ni kitendo  ambacho kinapaswa kulaniwa kwa nguvu zote.

Amesema  matukio hayo yamekuwa akiendelea  kila baada ya muda kwa watu kuharibu mindombinu ya maji kwa makusudi na kusababisha kuingizia hasa   serikali  kwa kutengeneza visima hivyo.

Afisa wa maji wilaya ya kaskazini ‘a’ dude juma ame  amesema licha ya kuwepo kwa ulizi  katika visima hivyo lakini kumekuwepo na tatizo la   wizi ambalo hufanywa na watu wasiopenda maendeleo.

Amesema visima vilivyo haribiwa husambaza maji kwa  wananchi wa nungwi,kidoti kihinani na matemwe ambapo wataweza kukosa maji kwa muda mfupi hadi hapo kutakapo fanyiwa matengenezo.