KUHIFADHI NYARAKA NA KUMBUKUMBU ZA SERIKALI.

Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora mh Seif Shaaban Mwinyi amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi ya nyaraka na kumbukumbu kulitumia vizuri, kulitunza pamoja na kulinda jengo la taasisi hiyo lililopo Chake chake ili kuifikiwa dhamira ya kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu za serikali.
Amesema ujenzi wa jengo hilo umefanywa kulingana na makubaliano ya mkataba ambao walitiliana saini na mkandarasi wa ujenzi huo.
Ameyasema hayo katika makabidhiano ya jengo la taasisi ya nyaraka na kumbukumbu lililofanyiwa ukarabati mkubwa uliogharimu shilingi milioni 200 ambalo zamani ilikuwa Ofisi ya mkuu wa Wilaya Chake chake Pemba.
Naibu katibu mkuu huyo ameendelea kusema kuwa kwa niaba ya Serikali kupitia wizara ya katiba sheria utumishi wa ummu na utawala bora amelipokea jengo hilo kama alivyokabidhiwa kwa ajili ya matumizi yaliyopangwa na kuwataka wajenzi hao kuzidisha ushirikiano kwa wizara kama ilivyokuwa katika kipindi cha mkataba.
Awali akitoa maelezo ya matengenezo ya jengo hilo la taasisi ya nyaraka Mshauri mwelekezi kutoka kampuni ya Sairala building consultancy Jafar Shauri Haji ameitaka wizara ya katiba sheria na utumishi wa umma na utawala bora kulifanyia jengo hilo marekebisho kwa wakati ili kuepuka.
Naye Injinia wa jengo hilo Moh’d Shehe Makame amewataka wakuu wanaosimamia taasisi hiyo kuziangalia athari zitakazojitokeza na kuwaarifu mapema badala ya kuzikusanya.
Wakati huo huo naibu katibu mkuu huyo amesema Serikali imeazimia kujenga kituo kipya cha kumbukumbu cha taifa cha Zanzibar katika eneo la Koani mkoa wa Kusini Unguja ambapo andiko la mradi huo limeshauzwa kwa wakandarasi