KUIHAMASISHA JAMII KUWA NA UPENDO KWA WATOTO WALIOKOSA MALEZI KUTOKA KWA FAMILIA ZAO

 

Kuwasili nchini kwa rais wa vijiji  vya  kulelea watoto  ulimwenguni  sos  ni   katika juhudi za kuihamasisha   jamii  kuwa na  upendo  kwa  watoto  waliokosa  malezi  kutoka kwa familia  zao ambao nao wana nafasi kubwa  ya kujenga taifa.

Akionesha  msisitizo   wa kuwajengea mazingira mazuri  watoto  hao  rais wa  sos ulimenguni, siddhartha  kaul,  akiungana katika  matembezi  ya pamoja  na watoto  wanaolelewa   katika kituo   cha  sos  zanzibar  kilipo  kwamchina.

Akizungumzia  juu ya ziara  hiyo  mkurugenzi  mkuu  wa sos  tanzania, anatoli rugaimukamu,  amesema  kutatoa  fursa  ya kutambua  mchango  wa kinamama   katika  malezi  ya watoto  ambao wamekuwa  wakijitolea  kwa moyo  wao wote  jambo ambalo  linapaswa  kuungwa mkono.

Aidha  amesema  kuwa sos  imepanga  mkakati  wa  kuhakikisha  kuwa  malezi wanayopatiwa watoto  hao  yanakuwa ni  sehemu  kuwajengea  msingi  imara wa maisha yao  ya  baadae.

Ziara  hiyo ya rais  wa sos ulimwenguni ni ya siku  mbili  hapa  zanzibar  ikiwa imelenga  kuwangalia mazingira  wanayoishi  watoto  hao  pamoja na  utoaji  wa zawadi  maalum kwa  mama  walezi.