KUIMARIKA KWA MIUNDO MBINU YA BARABARA NDIO CHACHU YA MAENDELEO

 

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuimarika kwa miundo mbinu ya barabara ndio chachu ya maendeleo kwa secta nyengine za kiuchumi kama vile, uvuvi, afya, kilimo utalii na biashara.

Kauli hiyo imetolewa na  waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais mh: mohd aboud mohd huko uwanja wa mpira mwane kwa niaba ya waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano  katika ufunguzi wa barabara ya madenjani mzambarauni ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra  kuelekea  maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi.

Mh: aboud amesema barabara ni kiungo muhimu katika maisha ya kila siku hasa kwa  wakaazi wa vijijini kwani inawarahisishia kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii, kuongeza ajira na kujipunguzia umaskini wa kipato.

Waziri wa ujenzi mawasiano na usafirishaji balozi ali karume amesema kufunguliwa kwa barabar hiyo kutasaidia kuchangia kukuza uchumi wa wananchi  na  kuwataka wananchi hao kuitunza barabara  hiyo.

Mapema akitoa maelezo ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita  5 katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, mawasiliano na usafirishaji mustapha aboud jumbe amesema kukamilika kwa barabara hiyo ni mipango ya serikali ya kuimarisha miundo mbinu.