KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO HASA KWA KAYA MASIKINI

 

Wakaazi na wakulima wa bonde la fuoni kibonde mzungu wameelezea kunufaika vyema na mradi wa tasaf awamu ya tatu kwa hatua wanazochukua za kuimarisha sekta ya kilimo hasa kwa kaya masikini.

Wakizungumza katika ufungaji wa mradi wa matengenezo ya bonde na ujenzi wa madaraja huko kibonde mzungu kupitia mradi wa tasaf awamu ya tatuwamesema  kuwepo kwa madaraja hayo kutarahisha kuyafikia mashamba yao na kulima kwa wakati hasa katika kipindi cha mvua kubwa za masika.

Wamefafanua kuwa kwa sasa wanalipwa shilingi elfu mbili na mia tatu kwa siku kiwango ambacho ni kidogo kulingana na kazi wanazofanya na kuomba kuongezwa ili kuongeza hamasa kwa wengine.

Akifunga mradi huo sheha wa shehia ya kibondeni nd iddi abdallah  amewataka wananchi na wakulima hao kuwa wasimamizi  na kuyatunza  madaraja hayo  yaweze kuwasaidia katika shuhuli zao za kila siku ili lengo la serikali la kuondoa umasikini liweze kufikiwa.

Msimamizi wa ukarabati wa bonde hilo nd maulid ramadhan saleh amesema kazi  hiyo iliyofanyika kwa miezi minne itawawawezesha wananchi kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata awali hasa wakati wa mvua masika.