KUIMARISHA SEKTA YA UTALII INAYOONEKANA KUPATA UFANISI

Kampuni ya kimataifa ya uhandisi wa miundombinu ya ujenzi ya garware yenye makao makuu yake mjini bumbay nchini india imesema ipo tayari kujenga ukumbi mpya wa kisasa wa kimataifa wa mikutano zanzibar iwapo watapata fursa hiyo.
Uwamuzi huo umekuja kufuatia serikali ya mapinduzi ya zanzibar kuwa na mpango wa ujenzi wa ukumbi wenye hadhi hiyo katika azma yake ya kuimarisha sekta ya utalii inayoonekana kupata ufanisi mkubwa.
Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi amemaliza ziara yake nchini india anatarajiwa kurejea nchini tanzania baada ya siku mbili.
Mkurugenzi miradi wa kamuni garware bwana deepakmenghnani alithibitisha hilo wakati wa mazungumzo yake na makamu wapili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi mwishoni mwa ziara yawiki moja ya ujumbe wa zanzibar hapo katika hoteli ya kimataifa yaeros mjini new delhi india.
Bwana deepak menghnani alimthibitishia balozi seif kwamba wahandisi wa kampuni ya garware iliyoanzishwa karibu miaka minane iliyopita wana
uwezo wa kujenga jengo la mikutano katika kipindi kisichozidi miakamitatu kwa mujibu wa uwezo wa mahitaji ya muhusika.
Amesema teknolojia rahisi inayotumika katika kampuni hiyo imewawezeshawataalamu na wahandisi wake kuendesha ujenzi wa mjengo tofauti ikiwemo
hospitali, skuli, ofisi za serikali na hata taasisi binafsi pamoja nanyumba za makaazi kwa bei inayomuwezesha mtu wa kawaida kumudu
kununua.Mkurugenzi huyo wa kampuni ya kimataifa ya uhandisi wa miundombinu yaujenzi ya garware alimueleza makamu wa pili wa rais wa zanzibar kwamba
taasisi hiyo ya ujenzi imekuwa ikishirikiana na wahandisi waliobobeakutoka nchini misri ili kuiwezesha kuwa na uhimili wa kimataifa.Bwana deepak menghnani alisema garware tayari imeshatoa huduma zaujenzi katika mataifa ya bukinafaso,sri lanka na dubai ndani ya
kipindi cha miaka minane tokea kuanzishwa kwake.Naye makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi alisema
serikali ya mapinduzi ya zanzibar iko tayari kuuandalikia barua yamualiko ujumbe wa viongozi wa kampuni hiyo katika muda mfupi ujao ili
kujionea mazingira ya zanzibar na kuona hatua gani zinastahikikuchukuliwa katika mwanzao wa kuelekea kwenye mpango huo wa ujenzi wa
ukumbi wa kimataifa.Balozi seif alisema zanzibar imeshafanikiwa kwa kiasi kikubwa katikauimarishaji wa sekta ya utalii lakini kinachokosekana kwa wakati huuni uwepo wa ukumbi wa kimataifa unaotoa fursa kwa wageni na hata nchirafiki kuelekeza nguvu zao za kufanya makongamano, mikutano na hata
vikao vya kimataifa.Balozi seif alisema ipo mikutano na baadhi ya semina za kimataifazinazopangwa kufanyika visiwani zanzibar lakini wajumbe wa mikutanohiyo hulazimika kuishi mbali na maeneo yao ya mikutano jambo ambalo huleta usumbufu wa kujipangia mambo yao mengine binafsi.