KUIMARISHA UKUSANYAJI WA MAPATO KWA URAHISI.

 

Wizara ya biashara viwanda na masoko imesema itahakikisha inaimarisha mifumo ya kusimamia biashara ili kukusanya mapato kwa urahisi.

Katibu mkuu wizara ya biashara viwanda na masoko bakari haji bakari amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni kuanza usajili kwa njia ya electroniki akiamini pia utapunguza udanganyifu wa taarifa za sekta hizo .

Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya mfumo wa usajili mradi huo unaoandaliwa na kampuni ya usajili ya nrd ya norway amesema mfumo huo utaanza kufanya kazi mwakani ambapo kwa sasa upo katika majaribio.

Mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya wakala wa usajili wa biashara na mali abdallah waziri amesema mfumo huo umekuwa ukitumia katika nchi mbalimbali duniani na kuongeza kuwa una umuhimu mkubwa kwa serikali katika kutambua taarifa za usajili kwa waanyabishara kwa urahisi zaidi.

Mshauri mwelekezi wa mradi huo avida laskas wa kampuni ni ya nrd  amesema mfumo huo utaondosha matatizo ya muda wa usajili pamoja na ulinzi wa taarifa .