KUIMARISHA ULINZI KWA MAHOTELI YANAYOPIGA MUZIKI RAMADHANI

Serikali ya wilaya ya kaskazini “a” imesema wataimarisha ulinzi kwa baadhi ya mahoteli yenye nia ya kutaka kupiga mziki mwezi huu wa ramadhani ili kuwaondoshea usumbufu wakaazi wa maeneo yanayo zungukwa na mahoteli hayo.
Akizungumza ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo hassan ali kombo amesema vitendo visivyokuwa na maadili ya kiislamu vinapaswa kukomeshwa ili kuepuka mmomonyoko wa maadili kwa mwezi huu mtukufu.
Mkuu huyo amesema serikali inajiandaa kukabiliana na wamiliki wa mahoteli wanaopinga agizo la serikali la kuzuia mkusanyiko wa watu wanaouza na kula kiholela kwa mwezi huu kwani inawezekana pia kukasababisha maradhi ya mripuko kutokea.
Kauli hiyo imekuja baada ya malalamiko ya wakaazi wa nugwi ya kuilalamikia hoteli ya kendwa rocks kuwa inataka kupiga mziki maarufu kama full moon part katika mwezi huu wa ramadhani.
Sheha wa shehia ya kilindi ali omar mussa amesema alipata malalamiko hayo kuwa hoteli hiyo inataka kupiga mziki mwezi huu na aliiandikia barua lakini hakupata majibu yoyote hivyo amewaomba wamiliki wa mahoteli yenye nia kama hiyo kuwacha mara moja kwani vitendo hivyo vinaweza kuleta usumbufu kwa wakaazi wa maeneo hayo.
Kwa upande wake darector meneja wa kendwa rock ali kilupi amesema kutokana na mwezi huu wa ramadhani wamesitisha kufanya full moon part hivyo amewataka wanaotaka kuja kwenye fullmoon part kutofanya hivyo na badala yake wasubiri mpaka mwezi wa ramadhani kuisha.