KUIMARISHWA MAJENGO YA KIHISTORIA KUMEKUWA NI KIVUTIO KWA WATALII NCHINI
Rais mtaafu wa zanzibar, dk. Aman abeid karumeAmetoa rai kuimarishwa majengo ya kihistoria Ndani ya mji mkongwe ambao umekuwa ni kivutio Kwa watalii wanaotembelea hapa nchini.
Dk. Karume amelazimika kutoa rai hiyo kufuatia uchakavu wa jengo la beit el ajaib, ambalo lina historia ya kipekee kwa nchi za afrika ya mashariki bara, na ni nyumba inayotunza kumbukumbu ya mambo ya asili katika visiwa vya zanzibar.Akizindua ukuta wa bahari wa mizingani uliojegwa kwa mara ya pili mwaka 2016 ambapo mara ya kwanza ulijengwa mwaka 1920, dk karume amesema kuimarika kwa majengo na miundombinu katika mji huo kutaongeza kasi ya ukuzaji uchumi kupitia sekta ya utalii na kuuongezea hadhi ya urithi wa kimataifa.Akiwasilisha taarifa ya kitaalamu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango, khamis mussa omar, amesema kiasi cha shilingi bilioni saba nukta sita tatu sita, zimetumika katika ujenzi huo uliojengwa kwa ushirikano kati ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar na benki ya dunia, chini ya kampuni ya sian brothers ya dar es salaam.Mwakilishi kutoka benki ya dunia amesema mazingira bora katika eneo hilo ni fursa muhimu ya kuvutia uwekezaji na ni sehemu salama kwa wananchi wanaotembelea hapo.Akizungumza katika hafla hiyo waziri wa fedha na mipango dk. Khalid salum mohamed, amesema kufanikiwa kwa mradi huo kumeipa nguvu benki ya dunia kufadhili awamu ya pili kuimarisha mji wa zanzibar.