KUIMARISHWA UHUSIANO WA KENYA NA ZANZIBAR WANANCHI WAFAIDI MATUNDA YA UMOJA HUO

 

 

 

Makamu wa Pili wa Zais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amesisitiza haja ya kuimarishwa uhusiano wa kenya na zanzibar ili wananchi wa pande hizo  waendelee kufaidi matunda ya umoja wao.

Akizungumza na waziri wa  utalii na mbuga za wanyama wa kenya mh, najib balala ofisini kwake  baraza la wawakilishi chukwani ,balozi seif amesema wananchi wa keya na zanzibar wanapaswa kukatakiina mema na kubadilishana uzefu katika mambo yenye tija.

Balozi seif akizungumza na waziri wa  utalii na mbuga za wanyama wa kenya mh najib balala ofisini kwake huko katika baraza la wawakilishi balozi seif amesemani vyema kila mmoja akaiga mambo mema na ya msingi.

amesema hali ya amani imezidi kuimarika kenya kwani amani ya kenya ni amani ya tanzania.

Hata hivyo balozi seif amesema lazima uhuru wa kenya uheshimiwe na utunzwe pamoja na ushirikiano kwa taifa.

Amesema bila ya amani na utulivu hakuna maendeleo hivyo lazima amani itawale na utulivu wa nchi uimarike.

Akizungumzia kuhusu utalii balozi seif amesema hivi sasa zanzibar utalii wake umeimarika katika  kila sehemu hivyo ni muhimu kuwa na ushirikiano katika kuimarisha utalii uliopo baina ya kenya tanzania na zanzibar.

Waziri wa utalii na mbunga za wanyama wa kenya mh najib balala  amesema zanzibar ina sifa njema katika bara la  afrika na  duniani kwa ujumla  katika kuimarisha utalii na kuwaleteea maendeleo wananchi wake.

Akizungumza na spika wa baraza la wawakilishi mh zubeir ali maulid mara baada ya kutambulishwa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi mh najib amesifu serikali ya mapinduzi ya zanzibar inavyoendesha shughuli zake za mkutano wa baraza la wakilishi  katika hali ya amani na utulivu.

Mapema waziri huyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa abeid amani karume  alipokelewa na waziri wa habari utalii utamaduni na michezo mh rashid ali juma na mwenyeji wake mh simai mohammed