KUINGIZWA KATIKA MITAALA MASOMO YA STUDY ZA MAISHA NA AFYA YA UZAZI YATAWASAIDIA WANAFUNZI KUJIELEWA

 

 

timu ya wataalamu ya wakuza mitaala na study za maisha  kutoka wizara ya elimu  wamesema kuingizwa katika mitaala masomo ya study za maisha pamoja na afya ya uzazi yatawasaidia wanafunzi kujielewa na  kujikinga na ukimwi na udhalilishaji wa kijinsia.

akifungua mafunzo hayo katibu mkuu wizara ya elimu  mafunzo ya amali  dr muslim hijja amesema  kutokana na tabia ya wanafunzi kujiingiza katika mapenzi wakiwa wadogo na kukatisha ndoto za maisha  hivyo  elimu hiyo itawakomboa kifikra na kuweza kupambana na matatizo hayo.

afisa ukimwi na mambo ya afya ya uzazi wa wizara ya elimu hasina salimu buheti na bi amina salum wamesema elimu hiyo itasaidia kuelekeza malezi yaliyo sahihi   na kuwaepusha wanafunzi na vishawishi mbalimbali ambavyo haviendani na mila na desturi na tamaduni za kizanzibari.

nae mtaalamu wa masuala ya elimu ya ukimwi kutoka unesco mathias herman amesema  wizara ya elimu  na unesco imekusudia kuwalinda  vijana  na masuala mbalimbali  yakiwemo ya udhalilishaji.