KUINUA KIWANGO CHA ELIMU MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 

Kamati ya mpango wa kuinua kiwango cha elimu mkoa wa kaskazini unguja imesema kutofuatwa kwa miiko ya uwalimu kwa baadhi ya walimu, uhaba wa walimu na ushuka kwa nidhamu kwa baadhi ya walimu kumetajwa kuwa miongoni mwa kushuka kwa kiwango cha elimu mkoani humo.

Akisoma ripoti ya uchunguzi ya kamati hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja mhe: vuai mwinyi mohamed , katibu wa kamati hiyo mohamed mzee chum amesema  uchunguzi uliofanywa  na kamati imebaini kuwa  mambo hayo yanazidi kuongezeka katika skuli za mkoa  jambo ambalo  husababisha kuporomoka kwa elimu mkoani humo.

Amesema kama hatua hazitochukuliwa kwa haraka kunaweza kuurejesha nyuma kimaendeleo mkoa huo.

Nae mkuu wa mkoa  amewashauri walimu wakuu  wa mkoa huo  kuwapendekeza walimu waliojitolea kwa muda mrefu waajiriwe ili kuziba pengo la uhaba wa waliu mkoani humo.

Wakichangia mada wanakamati hao wameshauri ofisi ya mkuu wa mkoa kuanzisha utaratibu wa kukutana na wazazi na walezi ili kuwaelimisha katika kushiriki masuala ya maendeleo ya kielimu kwa watoto wao.