KUIONDOA IRAQ KATIKA NCHI ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUINGIA MAREKANI

 

 

Rais wa marekani donald trump amesaini amri mpya inayozuia watu kutoka mataifa 6 yenye waislamu wengi kuingia nchini marekani, ikiwa ni marekebisho ya amri ya kwanza ambayo ilikwamishwa na maamuzi ya mahakama.

Katika marekebisho hayo mapya iraq imeondolewa kwenye orodha hiyo kutokana na kuchukuwa juhudi za kufanya uchunguzi wa matukio kadhaa na kubadilishana taarifa na marekani pamoja na kushirikiana katika vita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali wa is.

Afisa mwandamizi katika ikulu ya rais wa marekani amesema amri hiyo itaendelea kuweka marufuku ya hadi siku 90 ya raia wa nchi sita za kiislamu iran, libya, syria, somalia, sudan na yemen kuingia nchini humo.

Sheria hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 16 mwezi huu