KUISAIDIA SERIKALI KATIKA KUPUNGUZA ATHARI ZINAZOSABABISHA MAAFA

 

Mkurugenzi kamisheni ya kukabiliana na maafa  Zbar Shaabani Seif Mohd amewaomba wajumbe wa kamati ya kitaalam ya kukabiliana na maafa ya wilaya ya magharib/A kuisaidia serikali katika kupunguza athari zinazosababisha maafa kwa kutekeleza vyema  majukumu yao kwa mujibu wa nafasi walizonazo.

Mkurugenzi shabani ameyaeleza hayo katika ukumbi wa baraza la manispaa la magharib a/ akizungumza na wajumbe wa kamati ya kitaalamu ya wilaya hiyo ikiwa ni muendelezo wa vikao vyake vya ufuatiliaji na tathmini katika wilaya zote za unguja na pemba  amesema kamati zinawajibu wa kufanya vikao kila baada ya robo mwaka na kuandikia ripotizenye kuonyesha mchanganuowenye lengo la kuandaa mikakati imara itakayotatua athari zinazosabaishwa na maaafa

Aidha akibainisha athari kubwa zinazoikumba wilaya ya magharib A ni  tatizo la ujenzi holela usiozingatia viwango pamoja na njia za asili za maji kujengwa na kupelekea mafurikokwa mwaka huu wa 2017 zaidi ya nyumba 7018zimeathiriwa na mvua ukilinganisha na wilaya nyengine

Nae mkurugenzivwa baraza la man ispaa ya magharib A Said Juma Ahmada aamesema miongoni mwa athari hizo ndani ya wilaya yake ni watu kujenga katika maeneo ambayo hayajapimwahususani maeneo ya mabndeni na pindipo uongozi wa wilaya unapotaka kuchukua hatua inashindikana

muwasilishaji wa mada kutoka kamisheni ya maafa makane khatibu makame amelezea namna maafa yanapotokea zbar ambayo husababishwa na binadamu mwenyewe huku akitoa kauli mbiu makaazi salama punguza makazi katk maeneo hatarishi na punhguza kuhamaham kutokana na maafa

Na wajumbe wa kikao hichio wameitaka serikali ya wilaya hiyo kuchukua maamuzi sahihi ya kuwahamisha wale wote waliojenga katik maeneo hatarishi ambao hawakufuata taratibu za ujenzi kwa mamlaka husika dcu.