KUJADILI NA KUTAFUTA NJIA ZA KUKABILIANA NA MAAFA

 

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika visiwa vya unguja na pemba hadi kufikia terehe 22 mei mwaka huu athari mbali mbali zimejitokeza ikiwemo upotevu wa maisha , kujaa  maji  na kusababisha  baadhi ya nyumba za wananchi kutokukalika na kubomoka kwa miundombinu ya barabara.

Miongoni mwa waliopoteza maisha kufuatia mvua hizo ni watoto wa nne , mmoja kuzama katika bwawa la mtumwajeni , wengine wawili walifariki katika mashimo ya maji na mmoja alifariki baada ya kumponyoka dada yake katika eneo la mtoni kidatu.

Akitoa taarifa juu ya athari za mvua za masika kwa wajumbe wa kamati ya kitaalamu ya kupambana na maafa katika kikao maalum cha kujadili na kutafuta njia za kukabiliana na maafa  mkurugenzi mtendaji wa kamati hiyo makame khatib makame amesema kutokana na wingi wa kasi kubwa ya maji jumla ya nyumba 2,619 zimeathirika kati ya nyumba hizo ,2,557 zipo unguja na 44 pemba .

Katika miundombinu ya barabara zilizoathirika ni barabara ya mwanakwerekwe –fuoni , kibonde mzungu , mombasa kwa mchina ,darajani na barabara ya bububu kwa unguja na pemba barabara ya mkoani –chake , barabara ya mangwena na barabara ya mtambwe.

Kaimu mkurugenzi mamlaka ya hali ya hewa zanzibar said khamis said akitoa taarifa ya mamlaka ya hali ya hewa juu ya muelekeo wa mvua za masika amesema wastani kwa mwezi mei  kwa upande wa pemba wastani wa mvua ni mm 411 hadi kufikia tarehe 20 mwezi huu ilinyesha na kufikia mm 597.5 na unguja ni wastani wa mm 263 hadi tarehe 20 ilifikia mm 499.5.

Mvua za masika kwa mwaka wa 2018 zilianza kunyesha mwanzoni mwa mwezi machi katika maeneo mbali mbali ya visiwa vya unguja na pemba kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ya hali ya hewa tanzania, kanda ya zanzibar ilieleza kuwa mwelekeo wa mvua hizo zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani.