KUKABIDHIWA JENGO KWA WATU WALIOKUWA WAKITUMIA MADAWA YA KULEVYA.

 

Katibu mkuu ofisi ya makamu wa Pili wa Rais dk. Idrisa Muslim Hija amesema ameridhishwa na  ujenzi mzuri wa jengo lililojengwa na kampuni ya  al-hilal gereral trading co.limited kwa ajili ya  watu waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya.

Amesema jengo hilo  litakalokuwa la ghorofa limejengwa kwa umakini mkubwa na  watendaji wa kampuni hiyo ya kizalendo.

Akizungumza na  watendaji  na wasimamizi  katika hafla ya kukabidhiwa  ufunguo na cheti ikiwa  ni ishara ya kukabidhiwa  jengo hilo huko kidimni wilaya ya kati dr, idrisa amesema serikali itawajengea uwezo wa kujitegemea watu walioacha kutumia madawa ya kulevya.

Amesema ujenzi wa jengo hilo ni hatua ya mwanzo ya kuwaandaa vijana hao ambao ni taifa la kesho na kwamba serikali  itaendelea kubuni shughuli mbali mbali zikiwemo za ujasiriamali ili vijana hao waweze kuacha kutumia dawa za kulevya.

Naye mshauri muelekezi wa ujenzi  wa jengo hilo ndugu mbwana bakari juma  amesema ujenzi huo umechukua mienzi saba  kugharimu zaidi ya shilingi milioni mia tisa .

Mkurugenzi mtendaji  wa kampuni ya al-hilal hemed nassor  al-hilal amesema kapuni yake ina uwezo mkubwa wa kufanyakazi za ujenzi na kuwasihi watakaolitumia kulitunza vizuri.