KUKAMILIKA KWA KAZI YA UFUNGAJI WA MTAMBO WA BARAFU NDANI YA SOKO LA SAMAKI NA MBOGAMBOGA TUMBE

 

Kukamilika kwa kazi ya ufungaji wa mtambo wa barafu ndani ya soko la samaki na mbogamboga tumbe, kutawaondoshea tatizo la muda mrefu wavuvi na wachuuzi wa bandari ya tumbe.

Mkurugenzi idara ya maendeleo ya uvuvi zanzibar, nd. Mussa aboud jumbe, amesema kazi hiyo inatarajiwa kukamilika baada ya wiki mbili

Ambapo itahusisha ufungaji wa mtambo ambao utazalisha barafu tani tano ndani ya masaa 24 na itawasaidia wavuvi kuhifadhi samaki wao, sambamba na  ujenzi wa mnara wa tangi la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 5000.

Mkurugenzi mussa amesema hayo wakati  akizungumza na viongozi wa soko la samaki na mbogamboga tumbe wilaya ya micheweni, pamoja na viongozi wa serikali ya wilaya ya micheweni, juu ya kulifanyia ukarabati soko hilo na uwekaji ndani wa mtambo wa barafu pamoja na ujenzi wa paa.

Akiyataja matengenezo mengine yatakayofanywa katika soko hilo amesema ni ujenzi wa mtaro wakuoshea samaki na ubomowaja wa sehemu za madirisha kwa ajili kupitisha mwangaza ndani ya soko.

Amesema hali hiyo imekuja baada ya mkandarasi wa awali wa ujenzi wa soko hilo, kujenga kinyume na makubaliano ikiwemo suala zima la kuwezeka bati zinazopitisha muwangaza ndani ya soko.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya micheweni salama mbarouk khatib, amewataka wananchi wa tumbe kushiriki katika maendeleo ya soko hilo, ili liweze kuzalisha ajira mbali mbali ambazo zitawakomboa kiuchumi.

Katibu wa soko la tumbe suleiman hassan makame, pamoja na wavuvi wamesema kukamilika kwa kazi ya ufugaji wa mtambo huo utaweza kuongeza mapato ya soko la tumbe, kwani wataondokana na suala la kununu barafu kutoka kenya.

Matengenezo ya soko la samaki na mboga mboga tumbe a yanatarajiwa kugharimu kiasi ya shilingi milioni 10 hadi milioni 15 kwa makisio, fedha ambazo zinatolewa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar ikiwa ni ahadi ya rais wa zanzibar dk ali mohamed shein kwa idara ya maendeleo ya uvuvi zanzibar.