KUKOSEKANA KWA MAADILI YA KAZI KUMECHANGIA KATIKA KUVUJA KWA MTIHANI

 

Wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar imesema kukosekana kwa maadili ya kazi kwa baadhi ya watendaji wake, kumechangia katika kuvuja kwa mtihani wa kidato cha pili  ambao tayari umeshafutwa.

Tamko hilo la wizara limetolewa na naibu waziri wa elimu na mafunzo ya amali Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri, alipokutana na watendaji wa baraza la mtihani zanzibar, na kueleza kuwa kitendo hicho cha kukosa maadili kimeiweka jamii katika mazingira magumu kutokana na jitihada kubwa iliyochua ya kufanya maandalizi kwa watoto ili waweze kushiriki vyema katika mitihani yao.

Akionesha kutoridhishwa na tukio hilo la kuvuja kwa mtihani waziri wa elimu na mafunzo ya amali  Mh Riziki Pembe  Juma, amesema  mitihani ndio kipimo kinachopelekea taifa kupata wataalamu wenye sifa, hivyo  kuvuja kwa mitihani kutapeelekea kupata watendaji waliofaulu kwa kufanya udangayifu.

Mkurugezi mtendaji wa baraza la mitihani zanzibar Nd. Zuberi Juma Khamis, amesema wataandaa mikakati kuhakikisha kuwa tukio kama hilo halitojirudia.