KUKOSEKANA KWA USHIRIKIANO KWA KIKUNDI CHA WAFUGAJI WA MBUZI

Kukosekana kwa ushirikiano kwa kikundi cha wafugaji wa “mbuzi msitupumbaze’” mangapwani kunarudisha nyuma jitihada za kufikia malengo kwa baadhi ya wanakikundi kutokana na kuzidiwa na mifugo hiyo.
Ndugu kombo mati rajabu mfugaji wa kikundi cha msitupumbaze amesema kikundi chao kilianza na watu ishirini na kupokea mbuzi 45 kutoka taasisisi ya assp lakini hadi kufikia sasa kikundi hicho kina watu nane na kusababisha baadhi ya mbuzi kufa kutokana na kukosa huduma za malisho.
Sheha wa shehia ya mangapwani ndugu folabasi maridadi amesema sababu za wanakikundi hao kujitoa katika kikundi hicho ni kutaka kupata maendeleo ya haraka ikiwemo kiwango kikubwa cha uzalishaji wa maziwa
mkuu wa wilaya ya kaskazini b ndugu issa juma ali amewataka wananchi kuwa na msimamo wa kweli kabla ya kujiunga katika vikundi vya miradi ili lengo la serikali la kuanzisha miradi ya kuwakomboa wananchi kiuchumi liweze kufikiwa