KUKOSEKANA USHIRIKIANO KATI YA WATENDAJI WA BARAZA LA MJI WETE NA MADIWANI

Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mh. Omar khamis othman amesema kuwepo na mgogoro kati ya watendaji wa baraza la mji wete na madiwani wa baraza hilo unaweza kusababisha kupotea kwa mapato ya serikali.
Amesema kukosekana ushirikiano kati ya pande hizo kunakwamisha ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ambayo yanasaidia shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza na wadau hao katika ofisi zake wete, mh. Omar amesema serikali ya mkoa haitauvumilia kadhia hiyo na kwamba inaendelea kufanya uchunguzi wa mgogoro uliopo kati ya watendaji hao ili kuupatia ufumbuzi.
Amesema suala la madiwani kutoshirikishwa katika baraza hilo sio jambo la busara kwani wao ndio wanaopaswa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali katika maeneo wanayoishi, sambamba na kutekeleza miradi ya kimaendeleo kwa wananchi wao.
Kwa upande wa madiwani hao wamelalamikia kutoshirikishwa na watendaji wa baraza hilo wakati wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo na pale wanapohoji huambiwa hayawahusu.
Nae katibu tawala mkoa wa kaskazini pemba ahmed khalid abdalla amesema madiwani wanauwezo mkubwa wa kulibadilisha baraza hilo katika shughuli za kimaendeleo.