KULETA MAREKEBISHO YA TABIA NA MIENENDO MIZURI KWA KUNDI LA WATU WENYE ULEMAVU

 

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi alisema kwamba ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye  michezo mbali mbali ndio njia muwafaka inayoweza kuwasaidia kuleta marekebisho ya tabia na mienendo mizuri kwa kundi hilo la mahitaji maalum kutokana na kuwa michezo ni kinga na afya.

Amesema kundi la watu wenye mahitaji maalum wana uwezo na vipaji vya kufanya mambo makubwa endapo watapatiwa fursa za kutosha za kutumia vipaji vyao, ujuzi na uwezo waliotunukiwa na mwenyezi muungu.

Balozi seif ali iddi alieleza hayo kwenye tafrija ya kuwapongeza wanamichezo wenye ulemavu wa akili  hapo katika ukumbi wa sheikh idriss abdulwakil kikwajuni ambao walishiriki mashindano ya michezo ya watu wenye ulemavu    {specily olympic} iliyofanyika mwishoni mwa mwaka uliopita kwenye uwanja wa aman.

Amesema kwamba ni jambo zuri lililofanywa na idara ya watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na jumuiya na taaisi nyengine kuona ipo haja ya kuwakutanisha wanamichezo wenye ulemavu wa akili na kuwapongeza kwa aina ya kipekee.

Balozi seif  alisema serikali ya mapinduzi ya zanzibar itajitahidi kupambana na mitazamo hasi kwa kuendelea kuwaelimisha wananchi pamoja na kujenga mazingira mazuri zaidi, kupitia sheria, sera na miongozo kwa watu wenye ulemavu wa akili ili kupatab haki zao kama watu wengine.

Makamu wa pili wa rais wa zanzibar amewapongeza wazazi, walezi na wanamichezo wenye ulemavu kwa michango na mashirikiano ya karibu yaliyosaidia kufanikisha mashindano ya michezo  ya watu wenye ulemavu wa akili ambao vijana wa zanzibar walipata fursa ya kuvitangaza vipaji walivyonavyo.

Akitoa taarifa  katibu wa special olympic zanzibar tifli mustafa nahoda  alisema special olympic ni mpango maalum uliobuniwa kutoa nafasi ya kujitathmini kwa watu wenye mahitaji muhimu namna wanavyoshirikisha katika masuala ya kijamii.

Mustafa alisema mpango huu uliasisiwa nchini marekani mnamo mwaka 1968  kwa kujumisha nchi wanachama 180 ukishirikisha wanamichezo wapato milioni mbili.

Mustafa alieleza kwamba ushindi wa wachezaji wa zanzibar wenye mahitaji maalum umefanikisha ujenzi wa imani kwa wanajamii jinsi vijana wenye uklemavu walivyoshiriki vyema na hatimae kuonyesha uwezo wao wa kiajabu.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo naibu waziri wilaya ya nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais wa zanzibar mihayo juma nh’unga  alivikumbusha vyombo vya dola nchini kuendelea kutekeleza jukumu lao ikiwemo kuwachukulia hatua za kuwafichua watu wenye tabia ya kuwafisha watu wenye matatizo ya akili.

Naibu waziri nh’unga  alisema kundi la watu wenye mahitaji maalum lina haki kamili ya kupata fursa na nafasi kama wanavyopata watu wengine kwani bado wapo watu wanaohisi kwamba wale wenye ulemavu hawapaswi kushiriki michezo kutokana na hali zao.

Balozi seif  katika hafla hiyo alikabidhi medani hizo  kwa wachezaji 38 walioshinda mashindano hayo  ambao kati ya hao washindi 19  ni dhahabu, 9 shaba na 10 fedha.