KULIENDELEZWA KWA ENEO LA UWEKEZAJI MICHEWENI PEMBA

 

 

mwenyekiti wa kamati ya fedha, biashara  na kilimo  dk. mwinyihaji makame,  amesema  licha ya  jitihada  na mipango inayopangwa ya kuliendeleza eneo  la uwekezaji micheweni, lakini  bado  inaonekana hakujawa na na utayari  wa kuliendeleza eneo hilo.

Mwinyi Haji ameyasema hayo huko eneo la uwekezaji micheweni mara ya upokeaji wa taarifa ya uendelezwaji wa eneo hilo.

amesema  lazima  kufikiriwa  upya katika kuliendeleza eneo hilo  kutokana na kutokuwepo miundombinu  itakayowavutia  wawekezaji  ili kuweza kuwekeza .

akijibu baadhi ya hoja  zilizotolewa na wajumbe wa kamati  ya fedha,biashara   na kilimo  mkurugenzi sera,mipamgo na utafiti  dn. saumu  khatib haji  amesema eneo hilo  la uwekezaji  micheweni  ni  kati ya maeneeo makuu  ambayo  yako katika mpango wa kitaifa wa kukuza uchumi  na kuendeleza wananchi kimapato  huku  mgurugenzi kutoka zipa nd. ali bakar amesema serikali tayari  imeshatenga  fedha  za kutengeneza masta plain ya eneo hilo.

mapema akiwasilisha ripoti  ya  eneo la uwekezaji  micheweni  kaimu mkurugenzi  mkaazi mamlaka  ya uwekezaji  vitega uchumi  kisiwani pemba  nd. ali shaaban  amesema hatua  iliyofikiwa   katika uendelezaji wa eneo hilo  ni kuwepo mashirikiano baina  ya mamlaka  na wizara ya fedha   katika kuingiza miradi ya  upelekeaji wa miundombinu eneo hilo    katika miradi  ya kitaifa  kutokana na mamlaka   kukosa  fedha za uendeshaji.