KULINDA ASILI YA ZAO LA KARAFUU ILI IENDELEE KUBAKIA KATIKA UBORA WAKE.

Mkuu wa mkoa wa tanga mh. Martin shigella amesema atahakikisha analinda asili ya zao la karafuu ya zanzibar ili iendelee kubakia katika ubora wake.
Mh. Shigella amesema hayo wakati akizungumza na zbc katika ofisi zake tanga baada ya kikao cha kupanga mikakati ya kulinda asili ya karafuu zinazozalishwa ya zanzibar sambamba kuzuia magendo ya zao hilo kilichoshirikisha kamati za ulinzi na usalama za mkoa wa kaskazini na kusini pemba pamoja na tanga zilizofanya ziara ya kutembelea mkoa huo ya kudhibiti zao hilo.
Aidha katika kikao hicho mkuu huyo wa mkoa ameiyomba smz kufungua kituo cha kununulia karafuu zinazozalishwa tanga ili kutofautisha katika uuzaji kwenye soko la dunia.
Nae mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mh. Omar khamis othman na kusini mh. Mwanajuma majid abdalla wamesema wamekubaliana na uongozi wa mkoa huo kudhibiti magendo ya zao hilo kwa vitendo.
Akielezea historia ya zao la kafaruu ya zanzibar afisa kutoka zstc amesema serikali imejengwa na wasiwasi juu ya kuibuka uingizwaji wa karafuu za tanga na morogoro katika visiwa hivyo.
Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati hizo wametembelea bandari ya tanga kuzungumzia magendo ya karafuu na kuangali shughuli za maendele katika eneo hilo.