KULIPATIA UFUMBUZI TATIZO LA KUPASUKA KWA BOMBA LA MAJI

Naibu waziri wa wizara ya ujenzi, mawasiiano na usafirishaji mhe mohamed ahmada salum, ameahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la kupasuka kwa bomba la maji ili kupisha ujenzi wa ukuta wa bahari ya mizingani uendelee kama ilivyopangwa.
Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo amesema wizarahiyo kwa kushirikiana na wizara ya fedha pamoja na mamlaka ya mji mkongwe wanatarajia kulitengeneza bomba hilo hivi karibuni
Amesema ipo haja ya kulitengeneza bomba hilo kwa haraka ili kuzuia athari zinazoweza kutokea katika ujenzi wa ukuta huo.
Mtaalamu wa ujenzi wa ukuta wa mizingani kutoka kampuni ya seyan brothers, bw lourence gonsalves, amesema kutokana na matatizo yaliyojitokeza yamesababisha kuchelewa kukamilika kwa mradi huo.
Ujenzi wa ukuta wa bahari ya mizingani umegharimu zaidi ya shilingi bilioni saba unaotekelezwa na mradi wa zanzibar urban service projects zusp unaofadhiliwa na benki ya dunia