KUMEKUWA NA ONGEZEKO KUBWA LA MARADHI YA MOYO KWA WATOTO

 

Wizara ya afya imesema kumekuwa na ongezeko Kubwa la maradhi ya moyo kwa watoto wanaozaliwa Katika hospitali ya mnanzi mmoja na vituo vya afya Ambao hugundulika  kuanzia  watoto wa siku moja Hadi miaka 17.

Mkuu wa kitengo cha maradhi moyo hospitali ya mnazi mmoja  dk omar abdalla suleiman, amesema takwimu zinaonesha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaosumbuliwa na maradhi hayo na kulazimika   kuwahudumia wagonjwa 60 hadi 80 kila  siku kwa wanaofika kliniki wakisumbuliwa na  maradhi hayo.

Amesema  zaidi ya watoto mia nne tayari wameshapelekwa nchini izirail kwa  kupatiwa matibabu na wengine 268 wamepelewa india kwa kufanyiwa upasuaji na wengine hutibiwa hapa nchini.Aidha amesema wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vifaa  vya kuchunguzia maradhi hayo hali inayolazimu baadhi  ya wagonjwa kupelekwa tanzania bara kwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.Waziri wa afya hamad rashid mohamme amesema  wizara  itahakikisha kuwa vifaa vya kuchunguzia maradhi hayo vinapatikana ili wananchi waweze kupatiwa matibabu hapa nchini.