KUMEKUWA NA ONGEZEKO LA WATOTO NJITI WANAOZALIWA ZANZIBAR

 

Kumekuwa  na ongezeko la watoto  njiti  wanaozaliwa  Zanzibar ambapo katika  kipindi  cha  mwaka  huu  idadi  ya watoto  hao  imefikia 771 katika hospitali mbalimbali.

Katibu mkuu wizara ya afya Asha Ali Abdalla akizungumza na waandishi wa habari amesema  ongezeko hilo limekuwa kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma  huku idadi ya vifo vya watoto hao ikiongezeka wakati wanapozaliwa.

Amesema  kumekuwa na sababu mbali mbali ambazo husababisha  mama mjamzito kujifungua  mtoto njiti  ikiwemo shindikizo la damu, sukari  mfumo wa uzazi  pamoja na unene uliokithiri.

Daktari anaeshughulikia watoto katika hospitali ya mnazi mmoja  dk khamis ali abeid  amesema kuna vikwazo mbalimbali katika kuwahudumia watoto  njiti  ikiwemo ukosefu wa madaktari na wauguzi wa kutosha katika kuwapatia huduma stahiki na ukosefu wa hewa mambo yanayosabaisha kutokea kwa vifo vya watoto hao.

Nae daktari wa kitengo shirikishi cha  afya ya mama na mtoto  dk mariyam  bakari amesema kuwalea watoto hao ni kunahitajika ushirikiano ndani ya familia ili kuwawezesha kukua haraka wakiwa na afya bora.

Siku ya mtoto njiti huazimishwa kila ifikapo novemmba 17 ya kila mwaka ambapo ujumbe wa mwaka huu tufanye kazi kwa pamoja kumtuza mtoto njiti.