KUNAHITAJIKA MIKAKATI YA KUWAENDELEZA VIJANA KIELIMU

 

Mkuu wa Wilaya ya kaskazini “a” Hassan Ali Kombo amesema bado kunahitajika mikakati ya kuwaendeleza vijana kielimu ili kuzitumia fursa za maendeleo.

Akizungumza katika mafunzo ya kuimarisha mabaraza ya vijana mkoa wa kaskazini unguja amesema juhudi hizo zinapaswa kutekelezwa na  watendaji wa wilaya za mkoa ambao ndio wanaofahamu fursa nyingi zinazoweza kulifikia kundi hilo.

Akitoa mada ya ushirikishwaji wa vijana mjumbe wa jumuia ya maendeleo ya labayka abdalla mussa amesema vijana wengi wanashindwa kushiriki katika masuala ya maendeleo kutokana na kutofahamu sheria .

Katika hatua nyengine mtandao wa asasi za kiraia za mkoa wa kaskazini unguja umeyakagua mabaraza ya vijana yanayojishughulisha na ujasiriamali na kuahidi  kuendelea kuyaunga mkono katika shughuli zao.

Baadhi ya vijana wa mkoa huo wameomba serikali na taasisi nyengine kuwasaidia nyenzo za kutendea kazi ili malengo yao ya kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo