KUNDI LA MELI ZA KIVITA ZA MAREKANI

 

 

Kundi la meli za kivita za marekani, ikiwemo meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita, hazikuwa zinaelekea upande wa korea kaskazini kama ilivyoripotiwa awali, bali zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.

Jeshi la wanamaji la marekani lilikuwa limetangaza mnamo tarehe 8 aprili kwamba kundi hilo la meli likiongozwa na meli kubwa ya carl vinson lilikuwa likielekea rasi ya korea, kama hatua ya kuionya korea kaskazini.

Wiki iliyopita, rais donald trump pia alitangaza kwamba kundi kubwa la meli za kivita lilikuwa likitumwa eneo hilo.

Kufikia mwishoni mwa wiki, meli hizo zilikuwa zimesafiri umbali sana na rasi ya korea na zilikuwa zinapitia mlango wa bahari wa sunda kuingia katika bahari ya hindi.

Wakuu wa jeshi la wanamaji la marekani katika bahari ya pasifiki walisema jumanne kwamba walikuwa wamefutilia mbali safari ya meli hizo katika bandari ya perth.

Hata hivyo, wanajeshi wake walikuwa wamekamilisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyokuwa yamepangwa awali kati ya majeshi ya marekani na australia katika pwani ya kaskazini magharibi mwa australia.

Kundi hilo la meli sasa “linaelekea magharibi mwa pasiki kama lilivyoamrishwa”.