KUONGEZEKA KWA UCHUMI WA ZANZIBAR KUTOA FURSA ZA AJIRA

 

Kuwepo kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba za kuishi katika maeneo huru ya uchumi fumba kutawezesha kuongezeka kwa uchumi wa zanzibar, kutoa fursa za ajira kwa wananchi na itakuwa ni kivutio kwa kampuni za nje ya nchi kuja kuwekeza hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya uendelezaji wa miundo mbinu ya maeneo huru ya uchumi fumba kati ya serikali na kundi la makampuni ya bakhresa, waziri wa fedha na mipango dk. Khalid salum mohammed, amesema mradi huo mbali ya kuwanufaisha wananchi pia utaitangaza zanzibar kimataifa jambo litaongeza ukusanyaji wa mapato kwa wageni watakaofika hapa nchini kwa shughuli mbali mbali.

Aidha dk. Khalid amesema serikali imeridhishwa na ujenzi wa mradi huo na kwamba itaendelea kutoa ushirikiano ili kuona unafanikia lengo lililokusudiwa.

mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya bakhresa salim ali salim amesema wameamua kuwekeza katika eneo hilo la fumba kutokana na ramani yake kuwa ni kivutio katika masuala ya uwekezaji.

Mara baada ya utiaji saini mkurugenzi wa mamlaka ya kukuza vitega uchumi salum khamis nassor, amesema mradi huo wa ujenzi wa nyumba za kuishi utakuwa katika mfumo wa kibiashara ambao utahusisha ujenzi wa hoteli yenye hadhi ya juu ulimwenguni pamoja na kujengwa bandari ndogo

Uwekaji saini mradi huo unafuatia makubaliano yaliofikiwa miaka minne iliyopita ya uendelezaji wa miundo mbinu katika maeneo huru ya fumba uliosimamiwa na mamlaka ya kukuza vitega uchumi zanzibar zipa.