KUONGEZEKA KWA WAHITIMU WA FANI MBALIMBALI KUTASAIDIA UPATIKANAJI WA WATAALAM WALIO NA UBORA.

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohammed shein amesema kuongezeka kwa wahitimu wa fani mbalimbali nchini kutasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa wataalam walio na ubora.
Amesema kuwa hatua hiyo pia itasaidia kuweza kufikia lengo la serikali katika kuhakikisha zanzibar ya viwanda inafikiwa na kuendeshwa na wataalamu hao. akizungumza kwa niaba ya raisi katika mahafali ya 15 ya chuo kikuu cha zanzibar, waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh. Riziki pembe juma amesema serikali inafanya kila jitihada za kuinua sekta ya elimu nchini kwa kurahisisha upatikanaji wa mikopo ili wanafunzi wengi kuweza kufikia kiwango cha juu cha elimu.
Aidha waziri riziki ameutaka uongozi wa chuo hicho kuanzisha fani inayohusu masuala ya uvuvi wa bahari ili kupatikana wataalamu katika fani hiyo na kuweza kufikia malengo ya serikali katika kukuza sekta hiyo.
Nao wanafunzi waliohitimu masomo yao wameuomba uongozi wa chuo kuyatatua baadhi ya matatizo yanayokikabili chuo hicho ikiwemo uhaba wa vifaa vya kusomea ikiwemo compyuta pamoja na uhaba wa vikalio pamoja na walimu.
Jumla ya wahitimu elfu moja na 52 wametunukiwa vyeti kwa ngazi ya cheti, diploma , digree na master.