KUPATIWA KIWANDA CHA SUKARI ENEO LA ZIADA LA KICHWELE KWA AJILI YA KILIMO CHA MIWA.

Wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi imetii agizo la rais wa zanzibar la kuwapa kiwanda cha sukari mahonda eneo la ziada la kichwele kwa ajili kilimo cha miwa.
Agizo hilo lilitolewa naraisa wa zanzibar bna mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohamed shein katika ziara yake kiwandani hapo hivi karibuni, waziri wa kilimo mali asili mifugo na uvuvi mh. Hamad rashid mohamed amesema azma ya serikali ni kuhakikisha uwekezaji nchini unafikia kiwango kizuri.
Amesema eneo walilopiwa kiwanda cha sukari mahonda ni eneo la kichwele lenye ukubwa wa ekali 774 sawa na hekta 305 ambapo litakuwa la shughuli za ulimaji wa miwa.
Katibu mkuu wizara ya kilimo mifugo mali asili mifugo na uvuvi juma ali juma amesema lengo la serikali kutoa eneo hilo ni kukiwezesha kiwanda kufikia hatua nzuri ya uzalishaji zaidi.
Meneja wa biashara wa kiwanda cha sukari mahonda pranan shah amesema uongozi wa kiwanda umeafarajika baada ya serikali kuwapatia ardhi ya ziada ambapo wataweza kuzalisaha miwa kwa wingi.