KUPELEKWA KWA MADARAKA MIKOANI KUTAPUNGUZA MAJUKUMU KATIKA SEREKALI KUU.

 

 

Mwenyekiti wa kamati  ya ustawi   wa jamii   ya baraza la wawakilishi  mhe, mwinyi  haji makame,  amesema kupelekwa  kwa madaraka  mikoani  katika  baadhi  ya  wiazara  kutaweza kupunguza  majukumu katika serekali  kuu.Akizungumza    na  watendaji  wa  halmashauri  na baadhi ya  wafanyakazi wa wizara  ya  afya  na  elimu katika  ziara  ya kuangalia  majukumu  yao ya kazi,  amesema  sio jambo la busara kwa watendaji  hao  kufanya  udanganyifu   wakati wa utekelezaji wa yao, na  kuwataka  kuongeza bidii katika  utendaji wa kazi zao.Nae naibu waziri  ya nchi  tawala  za mikoa  serekali za mitaa  na  idara maalum  za   smz mh shamata   shaame  khamis,  amesema  serikali imeanza  kuweka  mikakati  ya mawasiliano  kuanzia   ngazi  za  madiwani  ambao  ni wasimamizi na wafatiliaji wa masuala ya kijamii katika wadi zao. .Hata   hivyo  mkuu wa  mkoa wa kaskazini  unguja   mh  vuai   mwinyi  muhammed, amesema mashirikiano  baina ya watendaji hao ndio  yatakayo fan ikisha  jitihada za kimaendeleo  kama zilivyokusudiwa.