KUPUNGUZA VIFO VINAVYOTOKANA NA UZAZI KWA AKINAMAMA NA MTOTO

 

Serikali  imo  katika  juhudi  za  kupunguza vifo  vinavyotkana  na  uzazi  kwa  akinamama  na  mtoto  hivyo  kuhamasisha  kuvitumia  vituo  vya  afya  kupata  huduma  za  haraka.

Katibu  mkuu wa  wizara  ya  afya  nd asha  ali abdulla  amesema  hali  hiyo  kwa  sasa  imeleta  faraja  kutokana na  ongezeko  l aasilimia  60  ya  akinamama kujifungulia  hospitali  kutoka  asilimia  40   ya  mwaka  2010 kunakochangia  kuondokana na matatizo  tofauti yanayotokana na  uzazi  .

Hayo  yamebaishwa  katika  ripoti  ya matokeo  ya  utafiti  wa  afya ya  uzazi  na  mtoto na  viashiria  vya  malaria mwaka  2015-2016 tanzania  na  utoaji  huduma  za afya mwaka 2014-2015 kwa  upande wa zanzibar  amesema  hali  inatisha  ongezeka  la   asilimia 16 kwa  wasichana  wenye umri  mdogo  kuanzia  miaka  15-19  kuzaa  kunakochangia kukatiza masomo    na kuhatarisha  maisha  yao.

Kwa  mujibu  wa  utafiti  wa  afya  uzazi  na  mtoto  uliowasilishwa  na  nd  fahima  muhammed  amesema uwezo  wa  kupata  watoto  kwa   pemba  upo  juu kwa  wastani  wa  watoto  saba  kwa  kila  familia  wakati  unguja  ni  watoto  wanne hali  inayoashiria  kutotumika  vyema  kwa njia  za  uzazi  wa mpango.

Mtakwimu  mkuu  wa serikali  bi mayasa  mahfoudh  mwinyi   amesema  matokeo  yaliowasilishwa  kutokana  na  utafiti  huo ni  muhimu  kwa  watunga  sera   watekelezaji  wa miradi  mbali mbali  katika  kufuatilia na kutathmini ili kuandaa  mikakati  mipya ya sekta  ya afya.