KUSHINDANISHWA KWA WANAFUNZI KATIKA SOMO LA SAYANSI KUTAWAJENGEA UWEZO WA KUWA WATAALAMU BORA

Waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh. Riziki pembe juma, amesema kushindanishwa kwa wanafunzi katika somo la sayansi, kutawajengea uwezo wa kuwa wataalamu bora wa taifa hapo baadae.h
Amesema taifa bado linahitaji kuwa na madaktari bingwa, wahandisi, marubani na wataalamu wengine, ambao kupatikana kwake kunatokana na vijana wanaofaulu vyema somo la sayansi.
Akizungumza katika shindano la kujibu masuali ya masomo ya sayansi kati ya skuli ya sekondari ya mikindani ya dole na fidelcastro ya pemba, mh. Riziki amesema mabli na kupata wataalamu lakini kumekuwa na upungufu wa walimu wa somo la sayansi, hivyo amewahimiza wanafunzi kuona umuhimu wa kupenda somo hilo.
Afisa miradi kutoka taasisi ya milele zanzibar foundation, eshe haji ramadhan, amesema wataangalia uwezekano wa kuongeza klabu za sayansi kupitia mradi wa stem, ili kuwaongezea hamasa wanafunzi kulipenda somo la sayansi.
Shindano limeandaliwa na jumuiya ya kumuendeleza kielimu mtoto wa kike fawe zanzibar, ambapo skuli ya fiedel castro imepata ushindi.