KUSHIRIKI KATIKA MAMBO YA KHERI ILI MALENGO YAFANIKIWE.

 

Waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kuongeza ushiriki wao katika mambo ya kheri ili malengo wanayoyapanga yafanikiwe.

Akizungumza baada ya kushiriki ujenzi wa msikiti unaotarajiwa kufanyika ijitimai ya kimataifa kidoti, rais mstaafu wa zanzibar mh. Amani Abeid Karume amesema bila ya ushirikiano mafanikio katika suala lolote yanaweza kuchelewa kutokana na kukosa nguvu ya pamoja.

Mh. Karume amesifu mwamko wa wanawake katika kufanikisha ijitimai hiyo ikiwemo kazi za ujenzi na kuwataka waumini wengine kutosita kutoa misaada yao ya hali  na mali ili kufanikisha ijitimai hiyo.

Mh. Karume pia ameupongeza uongozi wa jumuiya ya fiysabilillah tabligh markaz kwa kuwashajihisha waumini katika masuala ya kheir na kudumisha umoja wao.

Wakitoa ufafanuzi juu ya ujenzi huo viongozi wa jumuiya hiyo amir Ali khamis na Amir Mwalim Hafidh wamesema msikiti huo ni mkubwa kwa Zanzibar nzima  na unaweza kuswalia na  waumini wapatao elfu tano.

Ijitimai ya kimataifa inatarajiwa kufanyika mei kumi na mbili mwaka huu huko kidoti mkoa wa kaskazini unguja