KUSHIRIKIANA KWA KUIMARISHA ULINZI KATIKA SHEHIA ILI KUDHIBITI VITENDO VIOVU.

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini ‘b’ rajab ali rajab amewataka wananchi wa shehia ya kisongoni katika jimbo lakiwengwa kushirikiana kwa kuimarisha ulinzi katika shehia yao ili kudhibiti vitendo viovu.

Akizungumza na wananchi wa shehia hiyo amesema iwapo wananchi watakaa kwa pamoja na kubuni mbinu za  kuiweka salama shehia yao watafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa ni ulinzi wa mtu huanza na yeye mwenyewe binafsi kabla ya taasisi nyengine zenye majukumu hayo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya pia amepiga marufuku uwangushwaji na uuzwaji wa madafu ya minazi mirefu katika wialya hiyo  na kuwaruhusu wananchi watakapomuona mtu yoyote anauza madafu ya minazi mirefu wamkamate na kumfikisha katika vyombo vya sheria kwa ukamataji salama bila ya kumuumiza wala kuvunja sheria.

Ameseama madafu yanayoruhusiwa kuuzwa ni yale ya minazi ya kitamli tu na yoyote atakae kikiuka agizo hilo atafikishwa katika vyombo vya sheria kwa kuchukuliwa hatuwa zinazofaa.

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kaskazini ‘b’ makame mwadini silima amesema halmashauri yake ina mpango wa kuibuwa miradi ya maendeleo yenye kuleta tija na maendeleo endelevu kwa wananchi na kupunguza ziara za kimafunzo ambazo manufaa yake huwa ni ya muda mfupi.

Awali wananchi wa shehia ya kisongoni wakiwa katika mkutano wa pamoja na mkuu wa wilaya ya kaskazini b akiwa katika ziara za kutyembelea shehia nakusikiliza kero za wananchi wamelalamikia vitendo kadhaa wanavyofanyiwa na baadhi ya watu wasiowatakia mema ikiwemo wizi wa mazao na mifugo, baadhi ya watu kulewa na kufanya vitendo viovu, kukosa fidia za mazao yao yaliyoharibiwa kwa dawa ya kuulia magugu ya miwa sambamba na uwekwaji wa tagi kubwa la maji lilowekwa hivi karibu kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama wnanchi wa hapo na maeneo jirani.