KUSHUGHULIKIWA MAHITAJI MUHIMU YA KIJAMII YANAYOZOROTESHA MAENDELEO YA WAKAAZI WA VIJIJINI

Uongozi wa serikali katika mkoa wa kusini unguja umesema utashughulikia mahitaji muhimu ya kijamii yanayozorotesha maendeleo ya wakaazi wa kijiji cha ukongoroni ikiwemo miundo mbinu ya barabara.
Akizungumza na vijana wa kijiji hicho wakati wakitoa shukrani kwa serikali mkuu wa wilaya ya kati mashavu sukwa saidi amesema serikali itahakikisha huduma za afya, elimu na kilimo zitaondoa changamoto zilizopo vijijini.
Amewataka vijana hao kujiinua kiuchumi kwa kutumia miundo mbinu ya kisasa katika kilimo cha umwagiliaji maji, uvuvi na ufugaji wa nyuki kwa kutumia baraza ya vijana na vikundi vya ushirika.
Wakieleza changamoto zinazowakabili vijana hao wameiomba serikali kuhimiza kuimarisha huduma ambazo zitawarahisishia shughuli zao za kiuchumi pamoja na kupatiwa madaktari kutokana na huduma hizo kwa sasa zinafanywa na vijana wa kujitolea wa chama cha msalaba mwekundu red cross.
Mkuu wa mkoa wa kusini unguja dkt idrissa muslim hijja amesema serikali inafahamu matatizo yaliyopo lakini utekelezaji wake unakwenda sambamba na hali ya uchumi.