KUSHUKA KWA MAZAO MBOGA MBOGA NA BAADHI YA MATUNDA KATIKA SOKO LA MANISPAA YA MJINI

 

Kushuka kwa mazao mboga mboga   na baadhi ya matunda katika soko la manispaa ya mjini (mwanakwerekwe) kumeleta hasara kwa wakulima na wafanyabiashara hali amabayo inayopelekea kuharibika kwa mazao hayo.

Akizungumza na kamera ya biashara na uchumi mkuu wa soko hilo bwana. Makame khamis  ali ameiomba serikali kuwekeza katika secta ya viwanda ili wakulima na wafanya biashara waweze kupata fursa ya kusindika ili waweze kuepukana na hasara wanazokumbana nazo kwa sasa.

Naye bwana suleiman wasafi  mfanyabiashara  wa zao la tungule katika soko hilo hakuwa nyuma kueleza changamoto wanazozipitia kwa wakati huuambapo kwa sasa bei ya tungule imefikia  sh. Mia tano mpaka miatatu kwa kilo na boksi kununuliwa kwa sh. Elfu kumi mpaka elf nane .

Pi ameiomba serikali ijikite katika suala la kuwekeza kwa wingi katika sekta ya viwanda ili iwe tija kwao na kwa wakulima wa mazao hayo

Kwa upande wa pilipili boga na karoti nako hali bado ni tete ambapo ndug rajabu issa  amesema bei ya mazao hayo imeshuka sana na kupelekea kuuza kwa bei ya sh.600 kwa kilo kitu ambacho hakileti faida  yoyote bali wanafanya biashara kwa mazoea

Kamera ya biashara na uchumi haikuwa nyuma katika mazao ya matunda na ilipata fursa ya kuzungumza na bwana juma mbarouk ambaye ni mfanyabiashara wa tunda la tikiti maji   alisema kwa sasa wanashukuru bei ya zao hilo ipo juu tofauti na kipindi cha nyuma hali haikuwa ya kuridhisha

amesama kwa sasa tikiti maji unaweza kupata kwa sh.elfu nane wakati kipindi cha nyuma haikuwa hivyo  pia ameiomba serikali kuwapatia miundombinu ya viwanda ili waweze kusindika mazao hayo kitu ambacho kitaleta faida kwao na nchi kwa ujumla