KUSITISHWA UPIGAJI MZIKI NA UUZAJI WA POMBE KATIKA BAA YA NEW HAPPY ILIOPO KITUNDU

Mkuu wa mkoa mjini magahribi mhe ayoub mohammed mahmoud amesitisha upigaji mziki na uuzaji wa pombe katika baa ya new happy iliopo kitundu shehia ya mwakaje kwa kosa la kupiga muziki siku zote hali iliyokuwa ikiwakera wananchi.
Mhe ayoub amechukua hatua hiyo katika mkutano na wananchi wa shehia mbali mbali uliofanyika meli nane ikiwa ni mfululizo wa ziara zake za kukutana na wananchi kusikiliza malalamiko yao ili kuyapatia ufumbuzi na kulitaka jeshi la polisi kusimamia agizo hilo.
Amesema serikali ya mkoa wake haitamvumilia mtu yeyote atakaebanika anajihusisha na uendeshaji wa baa bila ya kufuata utaratibu wa sheria .
Wakizungumza katika mkutano huo sheha wa mwakaje na baadhi wananchi wameeleza baa hiyo imekuwa ikipiga mziki siku zote bila ya kufuata utaratibu na kuwa hatua ya kiongozi huyo sasa itawanyamazisha kilio chao.