KUTEKELEZA MIPANGO IMARA YA UENDELEZAJI WA MIJI

 

Idara ya mipango miji imeazimia kutekeleza mipango imara ya uendelezaji wa miji katika maeneo ya zanzibar kwa lengo la kunusuru zanzibar kuendelea na migogoro ya ardhi

Akizungumza katika mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya ardhi,mkurugenzi  wa mipango miji dr.muhammad juma  amesema zanzibar ina maeneo mengi yaliyokumbwa na migogoro ya ardhi kutokana na utumiaji mbaya wa ardhi usiokuwa na mipango maalum,hivyo katika kuondokana na kero hiyo maeneo 14 ya miji inatarajiwa kufanyiwa upangaji bora kuimarisha mji ikiwemo maeneo ya chwaka matemwe ambayo hivi sasa ndio inaendelea katika upangaji wake.

Wakielezea umuhimu wa mpango huo wadau walioshiriki katika kikao hicho wameshauri kutolewa elimu zaidi kwa jamii kuhusu kuzitumia fursa za mipango miji zitakapokuja kwani wao ndio walengwa wakuu katika utekelezaji wa kazi hiyo.

Maeneo makuu yaliyolengwa kunufaika na mpango huo ni pamoja na mkokotoni,nungwi,makunduchi,wete,na chakechake