KUTENGENEZA MABOMBA YALIYOPASUKA WAKATI WA KUTAYARISHA BARABARA

 

Mamlaka ya maji zanzibar  imesema itaendelea kutengeneza mabomba yaliyopasuka wakati wa kutayarisha barabara  huko fuoni mambo sasa ili wananchi wapate maji safi na salama.

Akizungumza nazbc vt  afisa uhusiano zawa  zahor sleiman amesema jitihada zinaendelea baadaya matengenezo ya barabara kuharibika mabomba ya kusambazia maji na  amewataka wanachi kuwawastahamilivu.

aidha afisa huyo wa  zawa  ametembelea maeneo ya kiaga na dole ambapo mamlaka yake inaweka mabomba ya kusambazia maji ili wanachi wawezekupata maji safi nasalama.

Shehawa shehia ya fuoni mambo sasa asiya omar moh,d

Awewasisitiza wananchi kujaza maji katika sehemu zao ili kuhakikisha hawapati usumbufu hadi matengenezo yatakapomalizika.

Wananchi wa sheia hiyo wamelezea matatizo yao na kushukuru serikali kwa kuwatengenezea barabara ambayo itawasaidia itkapomalizika.