KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI JUU YA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

 

Jumuiya  ya  uwezeshaji  kwa wote  imeandaa  kampeni  maalum  ya  kutoa  mafunzo   kwa wanafunzi  juu  ya  udhalilishaji   wa kijinsia  ulioshamiri hapa nchini baada ya kuona kwamba  vitendo  hivyo  vinazidi  kuiathiri  jamii  na taifa   tegemezi la hapo baadae.

Akizungumzia mpango  huo  mwenyekiti  wa jumuiya hiyo    giftness joseph  castico amesema  lengo  kubwa  ni kusaidia serikali katika kupunguza  vitendo  hivyo  kwani  athari kubwa inajitokeza kwa watoto na hasa wanafunzi ambao wao ndio tegemezi baadae hivyo kufanya hivyo kutasaidia kiasi kikubwa wanafunzi hao kuweza kujitambuwa.

Wakitoa mada katika skuli  mbali mbali za wilaya ya mjini  wakufunzi kutoka  juza  wamewataka  wanafunzi kujiepusha na mazingra yasiorafaiki kwao ambayo ndio chanzo  cha kufanyika matendo hayo .

Baadhi ya walimu wameupokea  mpango huo kwa mtazamo tofauti kwa kutoa wito kwamba elimu hiyo  inapotolewa  washirikishwe na wazazi majumbani kwani matendo mengi hutokea katika mazingira ya  jamii iliozunguuka maitaani