KUTOLEWA KWA MUDA VIBALI VYA USAFIRISHAJI WA MKAA NA KUNI

 

Mkuu wa  mkoa wa  kusini  Unguja mhe Hassan Khatib Hassan  ameruhusu  kutolewa kwa muda vibali vya usafirishaji wa mkaa na kuni baada ya wazazi wa kijiji cha ukongoroni  kuzuwia watoto wao wasiende skuli kama ni njia ya kupinga kuzuiwa wasisarifishe bidhaa hizo.

Wananchi wa vijiji vya charawe na ukongoroni kwa miaka kadhaa wamekuwa wakijishughulisha na ukataji wa kuni makaa na majengo ili kujikimu kimaisha

Mkuu wa mkoa ametoa maamuzi hayo katika kikao cha pamoja kilichowashirikisha watendaji wa mkoa huo wakiiwemo maafisa wa idara ya misitu na rasilimali zisizorejesheka zanzibar.

Hata amesema serikali inatafakari njia nyingine za kuwawezesha wananchi hao wasitumie msitu huo ili kuepusha kuumaliza na kusababisha balaa la kutokea jangwa.

Afisa mkuu idara ya misitu na mali zisizorejesheka  ndugu makame  kitwana  makame amesema wananchi wa ukongoroni wanapaswa kuheshimu makubaliano ya awali ya kuhifadhi rasilimali za misitu.

Wananchi kwa upande wao wameiomba serikali kuwatafutia mbinu mbadala itakayowezesha kuwaingizia kipato cha kijikimu na familiia zao ili kuweza kuondokana na tatizo la utumiaji wa rasilimali za misitu.