KUTOWAFUMBIA MACHO WATU WANAOFANYA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

 

Katibu tawala wa mkoa wa kaskazini unguja ndugu omar hassan masoud amewataka wananchi wa mkoa huo kutowafumbia macho watu wanaofanya vitendo vya udhalilishaji na badala yake wawaripotie kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumza katika mkutano wa kuhamasisha kupinga vitendo vya udhalilishaji katika shehia ya bumbwini misufini, omar amesema baadhi ya wananchi kuwaficha wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kwa kuwa ni ndugu katika familia zao jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa vitendo  hivyo.

Kwa upande wake kaimu afisa wa watu wenyeulemavu mkoa huo bi fatma jeilan amewataka wazazi na walezi kutowafungia ndani watoto wao wenye ulemavu na kuwakosesha fursa zinazotolewa na serikali kwani kufanya hivyo ni kuwadhalilisha watoto hao,

Wakichangia mada wanakamati ya kupambana na udhalilishaji shehia ya bumbwini misufini wamesema changamoto kubwa za kupambana na vitendo vya udhalilishaji ni kukosekana kwa elimu ya udhalilishaji kwa jamii.