KUVUNJWA MAENEO YALIYOKUWA YAKIKWAMISHA MAENDELEO YAO NA KUWAPA USUMBUFU

 

Wakaazi wa Bweleo wamesema wameridhishwa na hatua ya kuvunjwa maeneo yaliyokuwa yakikwamisha maendeleo yao na kuwapa usumbufu.

Maelezo ya wananchi hao yamekuja kufuatia  kuvunjwa kwa ukuta huko bweleo baada ya wananchi hao kumlalamikia mkuu wa mkoa mjini magharibi mhe, ayoub moahammed mahamoud alipofanya mkutano huko dimani.

Wamesema eneo lililojengwa ukuta huo lilikukua likitumiwa na wananchi kwa harakati mbali mbali za kimaendeleo na kijamii zikiwemo za uvuvi na kwamba ulikuwa ukiwapa usumbufu mkubwa.

Ukuta huo umevunjwa chini ya usimamizi wa  mkuu wa wilaya magharibi b kepteni silima haji haji na kuwaomba wakaazi wa wilaya hiyo kufuata taratibu wanapofanya  shuli za ujenzi ili kuepukana usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo wa kuvunjiwa.

Wakati huo huo baraza la manispaa magharibi b limefanya zoezi la kuvunja  ujenzi ambao haukufata taratibu za kisheria ya chuo cha afya mbweni ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na kamati ya ustawi wa jamii baraza la wakilishi baada ya mhusika kukaidi  kubomoa  mwenyewe.mwisho.