KUVUNJWA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU DODOMA

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe. Dkt. John pombe magufuli, ameivunja mamlaka ya ustawishaji makao makuu dodoma (cda) na kuagiza mali na shughuli zake kuhamishwa halmashauri ya manispaa ya dodoma.
Amesema ameamua kuivunja mamlaka hiyo na bodi yake ili kuondoa mgongano wa utoaji wa huduma kwa wananchi kati ya vyombo hivyo viwili pamoja na kuendana na mahitaji ya sasa.
Aidha, mhe. Rais magufuli ameagiza kubadilishwa hati zote za kumiliki ardhi zilizokuwa zinatolewa na cda kwa ukomo wa miaka 33 na kufikia ukomo wa miaka 99 kama katika maeneo mengine ili kuwavutia wawekezaji hasa wa viwanda.
Rais magufuli ameitia saini hati ya amri ya rais ya kuivunja mamlaka hiyo ikulu jijini dar es salaam mbele ya viongozi mbalimbali akiwemo makamu wa rais mhe. Samia suluhu hassan, waziri mkuu mhe. Kassim majaliwa.
Makamu wa rais mhe. Samia suluhu hassan na waziri mkuu mhe. Kassim majaliwa wamemshukuru mhe. Rais magufuli kwa uamuzi huo na wameahidi kusimamia utekelezaji wa maamuzi hayo.
Mamlaka ya ustawishaji makao makuu dodoma (cda) ilianzishwa tangu april 01. 1973.
“wananchi wa dodoma wamelalamikia tatizo hili kwa muda mrefu sana, hata nilipokuwa kwenye kampeni zangu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 walilalamika sana, sasa nimetekeleza niliyowaahidi, naamini kwa uamuzi huu malalamiko ya wananchi yatapata utatuzi na pia tutakuwa tumeondoa kikwazo cha umiliki wa muda mfupi wa ardhi uliosababisha wawekezaji kushindwa kujenga viwanda dodoma.
“sasa majukumu yote yanahamishiwa manispaa ya dodoma, sitaki kuendelea kusikia visingizio, mkajipange mambo yaende vizuri” amesisitiza mhe. Rais magufuli.